Kundi la watu likiwa na silaha wamevamia shamba ambalo linahusishwa na familia ya aliyekuwa Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta lililopo katika kaunti ndogo ya Ruiru ambapo nia ya uvamizi huo haikuweza kujulikana mara moja.
Tukio hilo, linadaiwa kutokea siku ya Jumatatu, Machi 27, 2023 ambapo kundi hilo la wavamizi wanaokadiriwa kuwa zaidi ya 100, kuvamia na kufanya uharibifu wa shamba hilo kubwa la Northlands lililo kando ya Barabara ya Mashariki.
Wavamizi hao, waliokuwa na silaha walikata miti kwa kutumia misumeno ya umeme na kutorosha idadi isiyojulikana ya mifugo kabla ya kuchoma sehemu ya shamba hilo kwa moto huku Wanahabari waliokuwa wakirekodi tukio hilo wakifukuzwa na wengine klujeruhiwa.
Shamba hilo la zaidi ya ekari 11,000 la Northlands City, liliwekwa kuwa mwenyeji wa kimbilio la mali isiyohamishika ambalo lilijumuisha maeneo ya makazi ya watu wenye kipato cha chini na cha juu, eneo la kilimo, eneo la viwanda na shule.
Inakadiriwa kuwa mradi huo kabambe ungegharimu hadi Shilingi 500 bilioni na wenye idadi ya watu wasiopungua 250,000 ambapo hata hivyo Waandishi wa habari waliokuwa eneo la tukio walirekodi kwa siri uvamizi huo baada ya kutishiwa mapanga.
Wengi wa wavamizi hao, walikuwa ni wanaume na walichukua kondoo, wengine walibeba mifugo na wengine walijaza kondoo kwenye magari yaliyokuwa yakipita na kufanya uporaji kwenye barabara kuu yenye shughuli nyingi.
Zifuatazo ni baadhi ya Picha za matukio (za juu na chini), zilizochukuliwa na Mwandishi wa The Standard, Silas Otieno.