Ushujaa wa kiungo kutoka nchini Uholanzi, Georginio Wijnaldum, umeiwezesha Newcastle Utd, kuchomoza na ushindi wake wa kwanza katika ligi ya nchini England mbele ya Norwich city hapo jana.

Wijnaldum, alifunga mabao manne miongoni mwa mabao sita yaliyoipa ushindi The Magpies ambao walikua nyumbani St James’ Park.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 24, alionyesha dhamira ya kweli ya kuisaidia Newcastle Utd katika mchezo huo, na alifanikiwa kufunga mabao manne katika dakika ya 14, 26, 66 na 85.

Mabao mengine ya Newcastle Utd, yalifungwa na Ayoze Perez pamoja Aleksandar Mitrović katika dakika ya 33 na 64.

Mabao ya kujipoza ya Norwich City yalipachikwa kimiani na Dieumerci Mbokani pamoja na Nathan Redmond katika dakika ya 20 na 34.

Ushindi huo umeisogeza Newcastle Utd katika nafasi ya 18 kwenye msimamo wa ligi ya nchini Engalnd kwa kufikisha point sita, ikitokea kwenye nafasi ya 20.

Kamati Ya Taifa Stars Yakutana Na Wadau Wa Soka
Lowassa Aimba Wimbo Mmoja na Mbowe Mbeya