Aliyekua nahodha na kiungo wa FC Barcelona Xavi Hernández, amesema anatamani kurejea kwenye klabu hiyo baada ya kuondoka mwishoni mwa msimu uliopita na kutimkia nchini Qatar kwenye klabu ya Al Saad.

Xavi aliwashangaza wengi baada ya kutoa kauli hiyo, lakini alipofafanua vizuri alieleweka baada ya kusema angepanda kurejea Camp Nou kama kama meneja.

Kiungo huyo ambaye atakumbukwa na mashabiki wa Barcelona, kutokana na mchango mkubwa alioutoa  na kufanikisha kutwaa ubingwa wa nchini Hispania mara nane pamoja na ubingwa wa barani Ulaya mara nne, amesisitiza jambo hilo kwa kuamini falsafa za Barca, zinampa uhuru wa kufikiria kurejea katika siku moja ya maisha yake.

Amesema asingependa kwenda popote pale ulimwenguni ili kutoa taaluma ya ufundishaji zaidi ya kurejea nyumbani Barcelona, na kuendelea kutoa mchango kwenye klabu hiyo ambayo ilimkuza tangu mwaka 1991.

Hata hivyo Xavi mwenye umri wa miaka 35, amekiri kuwepo kwa ugumu wa kupata nafasi ya kuwa meneja wa kikosi cha kwanza cha Barcelona kutokana na utaratibu uliowekwa klabuni hapo, japo aliendelea kusisitia anaamini anaweza kuifanya kazi hiyo.

Barcelona wamekua na mfumo wa kuwatumia wachezaji wake wa zamani katika nafasi ya umeneja, kwa lengo la kuendeleza mfumo wa soka wa klabu hiyo ambao kwa asilimia kubwa huwategemea vijana wanaokuzwa katika kituo cha La Masia.

Waliowahi kuwa wachezaji wa Barcelona na kisha kutangazwa kuwa memeneja miaka iliyofuata ni Pep Guardiola, Frank Rijkaard, Louis Van Gaal pamoja na Luis Enrique aliye kazini kwa sasa.

TFF Yatajwa Kuwa Chanzo Cha Upinzani Ligi Kuu
Video: Angalia Interview ya ‘kibabe’ ya Ruby kwenye The Playlist ya Times Fm