Mgogoro kati ya vikosi vya serikali na waasi wa M23, umesababisha makumi ya maelfu ya raia kukimbia mzozo huo huku wakimbizi wa ndani wakiamua kukata miti kwa ajili ya kuni na mkaa katika Hifadhi ya Virunga na kuharibu zaidi ya ekari 500.
Wakiongea kwa nyakati tofauti, wananchi hao wamesema, “tangu tufike kwenye kambi ya wakimbizi, misaada ya kibinadamu haijafika na idadi yetu inazidi kuongezeka mbugani na hata huu ukataji miti tunaoufanya ni kutafuta tu pesa ya chakula.”
Aidha, Wakimbizi wengi wamesema wametafuta makazi katika mbuga hiyo na kwamba wanyama wa kuvutia wakiwemo sokwe wa milimani sasa wamekuwa ndiyo marafiki kwao na katika muda wa chini ya miezi miwili zaidi ya ekari 500 za misitu, zimeharibiwa na kuwa mashina.
Mamlaka ya hifadhi ya Virunga, imesema itaendelea kukabiliana na wanamgambo wenye silaha wa eneo hilo ikiwa ni umepita mwezi mmoja tangu walinzi wawili kuuawa na mwingine kujeruhiwa na watu wanaoshukiwa kuwa ni wanamgambo wa m23.