Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Fortunatus Muslim amesitisha zoezi la uhakiki wa leseni lililoanza hivi karibuni hadi utakapotangazwa tena huku akitoa muda kwa madereva kwenda kusoma.

Muslim ametoa tamko hilo jijini Dar es Salaam wakati akiwa kwenye ziara ya kukagua utendaji kazi wa watendaji walio chini yake.

Aidha, kuhusu wanaokamatwa na makosa ya barabarani, Kamanda Muslim amesema gari yoyote itakayokamatwa kama ina madeni basi dereva wake asiandikiwe faini bali akamatwe na kufikishwa mahakamani.

“Dereva au gari itakayokamatwa kwa makosa ya usalama barabarani na kama anamadeni, asiandikiwe, apelekwe moja kwa moja mahakamani,”amesema kamanda Muslim

Waziri Kigwangalla apata ajali mbaya
Watumishi TRA wawekwa kikaangoni