Klabu ya Jang’ombe Boys ya visiwani Zanzibar inayoshiriki ligi daraja la Kwanza Kanda ya Unguja imemtambulisha, Hussein Sleiman Ali kuwa kocha mkuu mpya wa klabu hiyo kwa mkataba wa miezi sita.

Hussein anachukua mikoba ya kocha Rished Adolph aliyeondoka hivi karibuni kwa makubaliano ya pande zote mbili.

“Hussain Sleiman ni kocha mkuu Jang’ombe boys kutoka sasa kwa mkataba wa miezi sita.”

“Hii ni baada ya mwalim Rushed Adolph kupata timu yenye maslahi zaidi tumeridhiana pande zote mbili, tumevunja mkataba tumemruhusu.” Alisema Alawi Haidar Foum Katibu wa Jang’ombe Boys.

Kocha Hussain atasaidiwa na Issa Othuman Ali ( Amasha) ambaye nae pia amesaini mkataba mpya wa miezi sita kuendelea kusalia kati klabu hiyo.

Akutwa na mtambo wa kutengeneza silaha za moto
Twitter yafungia akaunti za wanaharakati wa kilimo