Mzunguko wa tano wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania (VPL) utafungwa kesho Jumanne Septemba 20, 2016 kwa mchezo kati ya African Lyon ya Dar es Salaam na Toto African ya Mwanza kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam. African Lyon inaingia uwanjani ikiwa na kumbukumbu nzuri ya kuilaza Mbao FC mabao 3-1 kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam wakati Toto African ilitoka kufungwa 1-0 na Tanzania Prisons ya Mbeya.

Raundi ya sita utapigwa Septemba 24, 2016 na Septemba 25, 2016 kwa michezo mitano siku ya Jumamosi na mitatu siku ya Jumapili. Siku ya Jumamosi JKT Ruvu itaikaribisha Mbeya City kwenye Uwanja wa Mabatini ulioko Mlandizi mkoani Pwani wakati Simba itakuwa mwenyeji wa Majimaji ya Songea kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Azam FC itasafiri hadi Mtwara kwenda kucheza na Ndanda kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona wakati Mwadui ya Shinyanga itakuwa mgeni wa Tanzania Prisons kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya na Mtibwa Sugar itakuwa mwenyeji wa Mbao FC ya Mwanza kwenye Uwanja wa Manungu ulioko Turiani mkoani Morogoro.

Siku ya Jumapili, Septemba 25, mwaka huu Ruvu Shooting inatarajiwa kuikaribisha Toto African kwenye Uwanja wa Mabatini ulioko Mlandizi mkoani Pwani huku Stand United ikiwa mwenyeji wa Young Africans katika dimba la CCM Kambarage wakati Kagera Sugar itakuwa jijini Dar es Salaam kwenye Uwanja wa Uhuru ikicheza na African Lyon.

Serengeti Boys Kuweka Kambi Nje Ya Nchi
Video: Kwanini uchumi wetu unakuwa lakini haupunguzi umaskini? - Prof. Ngowi