Kocha Mkuu wa klabu ya Simba SC Zoran Manojlović, ataanza kazi rasmi wakati wa maandalizi ya msimu mpya wa Ligi Kuu na Michuano ya Kimataifa kwa msimu ujao wa 2022/23.

Kocha Zoran alitangazwa na Uongozi wa Simba SC jana Jumanne usiku (Juni 28), baada ya kukamilisha taratibu zote za kuajiriwa klabuni hapo, huku akisaini mkataba wa mwaka mmoja.

Meneja wa Habari na Mawasilino wa Simba SC Ahmed Ally amesema Kocha huyo kutoka nchini Serbia ataendelea kuwa nje ya Tanzania hadi wakati wa maandalizi ya msimu mpya, ndipo atakapowasili Dar es salaam.

Amesema kwa sasa Kocha Zoran anafanya kazi kwa ukaribu na Uongozi wa Simba SC katika mchakato wa usajili wa wachezaji, ambao unaendelea klabuni hapo, hivyo anafahamu kila kitu kinachoendelea katika sekta hiyo.

“Kocha Zoran ataendelea kuwa katika mapumziko yake huko alipo kwa sasa, atawasili Dar es salaam siku chache kabla ya kuanza kwa maandalizi ya msimu mpya wa 2022/23,”

“Kazi kubwa anayoifanya hivi sasa baada ya kutangazwa kuwa Kocha Mkuu ni kushirikiana na Uongozi kufanya usajili wa wachezaji, ambao unaendelea katika klabu yetu, hivyo kila atakayesajiliwa atakua amepata baraka za kocha huyu.”

“Tunaamini wakati wa maandalizi Kocha atakua na wakati mzuri wa kukiandaa kikosi chake, kabla ya kuanza harakati za kusaka mafanikio ndani ya klabu yetu, ambayo kila mmoja anatamani yakirejea Msimbazi baada ya kupotea msimu huu.”

Amesema Ahmed Ally Kocha Zoran aliwahi kufundisha kwenye klabu za Al Hilal ya Sudan kati ya mwaka 2020-21, Primeiro de Agosto-Angola (2017–2019), Wydad AC-Morroco (2019–2020), CR Belouizdad-Algeria (2021) na Al-Tai-Saudi Arabia (2021).

Rekodi za vifo vya raia nchini Syria inatisha
Simba SC yafafanua mkataba wa mwaka mmoja