Katika hali isiyo ya kawaida, mchezaji wa timu ya Trabzonspor ya Uturuki alimpiga kadi nyekundu refa wa mchezo kati ya timu yake na Galatasaray, uliofanyika Jana (Februari 21) ambapo timu yake ilifungwa 2-0.

Mchezaji huyo anayefahamika kwa jina la Salih Dursun, alionekana kuchukizwa na kadi nyekundu aliyopigwa mchezaji mwenzake kwa kucheza faulu katika eneo la penalti wakati ambapo timu yake imeangukia pua. Refa wa mchezo huo alimpiga kadi nyekundu Luis Cavanda katika dakika ya 86 ya mchezo huo.

Wachezaji wa timu hiyo walimsonga muamuzi Deniz Bitn wakimlalamikia kwa uamuzi wake, ndipo Dursun alipomnyakua kadi nyekundu na kumnyooshea huku akimuonesha nje kwa maana kwamba muamuzi huyo anatakiwa kutoka nje ya mchezo huo.

Hata hivyo, umauzi wa Dursun ulimponza baada ya Muamuzi huyo kumuondoa uwanjani kwa kadi nyekundu hivyo kufanya timu yake kuwa pungufu ikiwa na wachezaji saba pekee.

Angalia hapa:

Magufuli afanya ziara ya kimyakimya kivukoni
Mugabe agonga chumvi nyingine Kimyakimya