Ajali mbaya ya basi imetokea wilaya ya Kiryandongo nchini Uganda na kusababisha vifo vya wa 19 na wengine 25 kujeruhiwa vibaya ambapo wamekimbizwa katika hospitali ya wilaya ya Kryandongo
 
Gazeti la Daily Monitor nchini Uganda limeripoti kuwa basi linalomilikiwa na kampuni ya Gaagaa ambalo lilikuwa safarini kutoka wilaya ya Lira liligonga trekta ambayo ilikuwa inaelekea kitongoji cha Karuma wilaya ya Kiryandongo.
 
Aidha, taarifa kutoka Jeshi la Polisi zimesema kuwa basi hilo liligonga trekta kwa nyuma na baada ya hapo, kupoteza muelekeo na kusababisha kugongana uso kwa uso na gari la mizigo lililokuwa limebeba kreti za bia, ambalo lilikuwa linatokea Kampala.
 
“Watu 19 wamepoteza maisha papo hapo wakiwemo madereva watatu. Watu wengine 25 wamekimbizwa hospitali na kulazwa katika hospitali ya Kiryandongo,” amesema msemaji wa polisi mkoa wa Albertine, Julius Hakiza
 
  • Mkuu wa Jeshi la Polisi awaamuru wananchi kuwapiga mawe Polisi
 
  • Masharti magumu yaliponza Kanisa, sasa kuburuzwa Mahakamani
 
  • Rushwa yazidi kuitafuna serikali ya Kenyatta
Hata hivyo, Uongozi wa hospitali ya Kiryandongo umesema kuwa mpaka Jumamosi asubuhi, walikuwa tayari wamepokea miili 23 katika sehemu ya kuhifadhia maiti

Mambosasa aibuka na Dk. Shika kurejea na mabilioni
Wanawake wawili wakubaliana kufunga ndoa na Ronaldinho mwaka huu