Basi la Kampuni ya BEST LINE lililokuwa likitokea Mbeya kuelekea Mwanza limepata ajali ya kupinduka leo Machi 28, 2018 katika Kijiji cha Ilongo kilichopo mkoani Mbeya.

Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya, Mohamed Mpinga amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo huku akisema kwamba hadi sasa bado hakuna taarifa za vifo, isipokuwa majeruhi tu.

Amesema kuwa chanzo cha ajali ni lorry lililokuwa linatoka Njombe kuelekea Mbeya lilikuwa linaovateki magari mengine na basi la Bestline lilikuwa linatoka Mbeya kuelekea Mwanza likiwa upande wake.

“Baada ya kuona watagongana uso kwa uso dereva wa basi akaona atoke nje ya barabara na kwenda kutumbukia kwenye mtaro kushoto,”amesema Kamanda Mpinga.

Shein awaapisha viongozi leo
Tanzania Prisons yaitumia salamu JKT Tanzania

Comments

comments