Siku chache baada ya Ali Kiba kuchaguliwa kuwa mmoja kati ya wamiliki na wakurugenzi wa kampuni ya muziki Afrika ya Rockstar4000 na Rockstar TV, leo ameanza kazi kwa kasi kumsainisha mkataba Ommy Dimpoz.

Ommy Dimpoz ambaye ni bosi wa PKP, ameweka wazi taarifa za kusaini mkataba huo na kuwa mwanafamilia rasmi wa Rockstar4000, leo kupitia akaunti yake ya Instagram.

”My fans! its official, I’ve signed with the biggest music company in Africa *RockStar4000 as my new manegementteam and with the premiere Pan Africa Music Entertainment content & News Channel,” ameandika Ommy Dimpoz.

Hili ni shavu lingine zito kwa Ommy Dimpoz kutoka kwa King Kiba baada ya kumsaidia kumtambulisha kwa nguvu kwenye mkondo mkuu wa muziki wa Bongo Fleva kwa ngoma yake iliyomtambulisha ‘NaiNai’.

Tazama video aliyoipost Mkurugenzi wa RockStar4000, Alikiba ikionesha jinsi Ommy Dimpoz alivyosainishwa mikataba katika kampuni hiyo kubwa ya muziki Afrika.

Wema Sepetu awaonya wajawazito kupiga picha za utupu
China yaikingia kifua Korea Kaskazini dhidi ya 'makombora' ya Marekani