Ali Kiba ameeleza kushangazwa na uamuzi wa waandaaji wa tuzo za MTV Europe Music Awards (EMA) kutompa tuzo ya Best African Act ingawa aliongoza kwa wingi wa kura. Tuzo hiyo ilienda kwa Wizkid.

Akifunguka katika kipindi cha Jahazi cha Clouds Fm, Ali Kiba alisema kuwa yeye binafsi pamoja na mashabiki wameshangazwa kutoipata tuzo hiyo kwani kura za mashabiki ziliokuwa zinaonesha wazi.

“Kwa hiyo mashabiki walikuwa wanataka kujua ni kitu gani kilikuwa kimetokea at least tuweze kupata hata voice ya explanation kiundani ili kila mtu afahamishwe ni kitu gani au ni vigezo gani wametumia kufanya mimi nisishinde ile tuzo. Hiko ndio kitu tunachosubiria na menejimenti yangu,” alisema.

Mkali huyo wa ‘Aje’ alikuwa akiwania tuzo hiyo pamoja na Wizkid (aliyeshinda), Black Coffee, Olamide na Cassper Nyovest .

Wabunge wapinga kupangiwa posho, waridhia wembe unyoe za watumishi Serikalini
Majaliwa aiomba uingereza kuwekeza zaidi nchini