Msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka Tanzania na mkurugenzi mpya wa kampuni kubwa ya kusimamia muziki Afrika ‘RockStar4000’ AliKiba ameamua kuzima kelele za mashabiki wake waliokua wakihoji kuhusu kutoa wimbo mpya.

Alikiba amethibitsha kuwa hivi karibuni anatarajia kutoa kichupa chake kipya na msanii maarufu toka Nigeria ambaye hivi sasa anafanya vizuri na kibao chake cha ‘If’, Davido.

King kiba amevujisha fununu hizo kupitia akaunti yake ya Snapchat, ambapo imeonekana Alikiba akiwa na staa huyo wa Nigeria Davido  wakiwa pamoja wakifanya kitu wakiwa na furaha, King Kiba alithibitisha kuwa kazi yao itakuwa tayari karibuni ”Coming Soon”.

Kupitia taarifa aliyoitioa King Kiba pindi alikihojiwa na Clouds FM, ameeleza kuwa ngoma ambayo ingefuata baada ya Aje ni ngoma ya kushitukiza ambayo hatomshirikisha msanii yeyote.

Kwa tafsiri hiyo Kiba amewaandaa vyema mashabiki wake kusubiria akishusha nyimbo zake kwa mashabiki wake waliokuwa wakimngojea kwa muda mrefu.

 

Mdee azidi kusota lupango, sakata lake lazidi kuibua mijadala
Uhuru Kenyatta ainyooshea kidole Mahakama, atoa onyo kali