Shirikisho la soka nchini Algeria limempa ajira kocha kutoka Hispania Luis Lucas Alcaraz González, kuwa mkuu wa benchi la ufundi la timu ya taifa ya nchi hiyo.

Alcaraz anakua kocha wanne kuajiriwa na shirikisho hilo ndani ya miezi 13 iliyopita, baada ya waliomtangulia kutimuliwa/kujiuzulu kazi kwa kushindwa kufikia malengo ya kufanya vyema katika michuano ya kimataifa.

Alcaraz amepata bahati ya kupewa ajira kama kocha mkuu, ikiwa ni siku tano baada ya kutimuliwa kazi kama meneja wa kikosi cha Klabu ya Granada, ambayo inaburuza mkia katika msimamo wa ligi ya nchini Hispania (La liga).

Kocha huyo mwenye umri wa miaka 50, amechukua nafasi ya Mbelgiji Georges Leekens ambaye alilazimika kujizulu siku chache baada ya Algeria kutupwa nje kwenye fainali za mataifa ya Afrika, zilizounguruma mwanzoni mwa mwaka huu nchini Gabon.

Kocha kutoka nchini Ufaransa Christian Gourcuff alifukwa kazi nchini Algeria April 2016, na nafasi yake ilijazwa na Milovan Rajevac ambaye alitangaza kujiuzulu baada ya kukiongioza kikosi cha The Desert Warriors katika michezo miwili.

Hata hivyo haikuwa kazi rahisi kwa viongozi wa juu wa shirikisho la soka nchini Algeria kufanya maamuzi ya kumpa ajira Alcaraz na kumtangaza saa kadhaa baadae, kutokana na orodha ya makocha wengine walioomba nafasi hiyo kutoka Hispania.

Image result for Luis Lucas Alcaraz GonzálezLuis Lucas Alcaraz González

Walioomba nafasi hiyo alikua Joaquin Caparros, Aitor Karanka ambaye alikua meneja wa klabu ya Middlesbrough ya England kabla ya kutimuliwa mwishoni mwa mwezi uliopita.

Kazi ya kwanza ya Alcaraz itakua Juni 13 mwaka huu, ambapo Algeria itacheza mchezo wa kuwania kufuzu fainali za Afrika (2019 AFCON) dhidi ya Togo mjini Blida, Algeria.

Algeria imepangwa kundi D sambamba na timu za Benin, Togo na Gambia.

Katika harakati za kuwania fainali za kombe la dunia 2018, Algeria itapambana na Zambia Agusti 28, na katika msimamo wa kundi B The Desert Warriors wanaburuza mkia wa kundi hilo kwa kuwa na point moja.

The Desert Warriors tayari wameshacheza michezo miwili, ambapo walilazimisha sare ya bao moja kwa moja dhidi ya Cameroon na kisha wakakubali kichapo cha mabao matatu kwa moja dhidi ya Nigeria.

Video: DC Mjema atangaza neema kwa wananchi Ilala
Didier Drogba Anunua Hisa Za Phoenix Rising FC