Imeripotiwa kuwa aliyekuwa kocha wa Yanga na sasa Zesco United, George Lwandamina, ameteuliwa kuwa mshauri wa masuala ya ufundi wa timu ya Taifa ya Zambia.

Maamuzi hayo yamekuja ikielezwa  kuwa Shirikisho la Soka nchini Zambia limeridhishwa na utendaji kazi wake mzuri ndani ya klabu.

Lwandamina ameiongoza Zesco United katika mechi za ligi msimu huu kwa kucheza mechi nane ikiwa kileleni mwa msimamo kwa kuwa na alama 22.

Katika alama hizo 22 kileleni, Zesco hawajapoteza mchezo wowote ule na badala yake wameenda sare moja.

Uingereza: Waziri Boris atengua kauli
Serikali yawataka walemavu kusimama na kujipambania

Comments

comments