Benki ya TIB imetoa taarifa ya kusikitishwa kwake na kitendo cha dereva wa gari inayomilikiwa na benki hiyo yenye namba za usajili SU 38431 cha kubeba mbuzi kwenye tairi ya akiba iliyopo nyuma ya gari.

Kwenye taarifa hiyo ambayo imetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya TIB Tawi la Mlimani City, imeeleza kuwa ni kwa namna gani dereva huyo ametumia mali ya umma vibaya, na pia kukiuka haki za wanyama.

Benki hiyo imesema kuwa itamchukulia hatua stahiki dereva huyo, ambaye alikuwa akiendesha gari hilo kutoka Mwanza kuelekea jijini Dar es salaam.

 

 

Video: Manispaa ya Kinondoni yawahimiza wasanii kujitokeza na kujisajili TACIP
CCM kwachafuka, kada ajiokeza hadharani, atangaza nia 2020

Comments

comments