Kenya, Ruth Kamande ni binti aliyewahi kushinda taji la U-miss Lang’ata Prison 2016 ambaye mapema jana amehukumiwa kifo mara baada ya kukutwa na hatia ya kuua kwa kutaka akiwa na umri wa miaka 21.

Mnamo 2015 binti huyo aliingia katika mgogoro mzito wa kimapenzi na aliyekuwa mpenzi wake, Farid Mohamed na kujichukulia uamuzi wa kumuua kwa kumchoma mpenzi wake visu 22.

Ndugu wa marehemu Farid Mohamed wamefurahishwa na hukumu  iliyotolewa na mahakama ya kumuhukumu kifo mlimbwende huyo kwani wameona mahakama imetenda haki.

Aidha jaji aliyetoa hukumu hiyo, Lessit amesema hukumu hiyo ni funzo kwa vijana ambao huchukua hatua kama hizo wakati mahusiano yanapofeli.

Hata hivyo matukio kama hayo yamekithiri sana hapa nchini ambapo kumekuwa na mauaji mengi yanayotokana na wivu wa mapenzi, hivyo endapo hatua kama hizo zitaendelea kuchuliwa na hapa nchini kuna uwezekano mkubwa wa kutengeneza hofu kwa watu na kupunguza matukio hayo.

Kwenye picha kushoto ni mwanadada Ruth Kamande aliyehukumiwa kifo, na kulia ni aliyekuwa mpenzi wake marehemu Farid Mohamed aliyechomwa visu 22 na, Ruth Kamande mara baada ya kuingia katika mgogoro.

 

Wema Sepetu alipa faini ya hukumu ya kesi yake
Neymar Jr aikataa Real Madrid

Comments

comments