Katika hali isiyo ya kawaida, wakati dunia nzima ikizizima kumshukuru mama na kumuombea kwa kuleta uhai wa kila mmoja wetu, raia wa Marekani aliyetajwa kwa jina la Joshua Lee Webb aliitumia siku ya mama duniani kumuua kikatili mama yake mzazi aliyekuwa akiishi naye, Tina Marie Webb.

Lee Webb

Kwa mujibu wa taarifa iliyoripotiwa na USA Today, baada ya mauaji hayo Webb mwenye umri wa miaka 36 alibeba kichwa cha mama yake na kuzunguka nacho kwenye mgahawa mmoja na kisha kumchoma kisu mtu mwingine aliyetajwa kwa jina la Michael Wagner.

Hata hivyo, wananchi walifanikiwa kumkamata Webb na kutoa taarifa Polisi katika eneo la Oregon ambao walifika na kumtia nguvuni. Jeshi la polisi la eneo hilo limeviambia vyombo vya habari kuwa tayari wamemfungulia mashtaka ya mauaji ya mama yake pamoja na jaribio la kumuua Wagner. Walisema Wagner alikimbizwa hospitalini ambako anaendelea na matibabu.

Webb anashikiliwa katika mahabusu ya eneo la Clackamas, kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Jumatatu wiki hii na wa kitengo cha polisi.

Wakati huohuo, polisi walieleza kuwa walipokea simu kutoka kwenye nyumba ya Webb iliyoko Colton, umbali wa maili 12 kutoka eneo waliloukuta mwili wa mama yake Webb.

Polisi hawakutoa maelezo ya kina ya sababu zilizopelekea mauaji ya kikatili ya mama Webb, lakini uchunguzi juu ya tukio hilo unaendelea.

Hili ni tukio baya kutokea hususan katika siku hiyo ambayo kila mmoja aliitumia kumshukuru zaidi mama yake na kumpa ujumbe mzuri. “Hakuna kama mama, mama ndiye chanzo na mhimili wa uhai wetu. Heshima zote kwa mama.”

Magazeti ya Tanzania leo Mei 20, 2017
Video: Tumekubaliana tumwache Meya akae polisi-Lema

Comments

comments