Mcheza tennis kutoka Uingereza, Andy Murray amejitosa kulizungumzia sakata la usawa wa kijinsia katika mchezo huo ambalo lilichukua nafasi kubwa mwishoni mwa juma lililopita, mara baada ya kukamilika kwa michuano ya Indian Wells Masters.

Murray , ambaye ni namba mbili kwa ubora duniani upande wa wanaume, amesema hakuna sababu ya jambo hilo kuzungumzwa kwa kujaribu kutenga jinsia, kwa kuamini jinsia moja ni bora zaidi kuliko nyingine kwa kuangalia vigezo vya kupata zawadi kubwa zaidi.

Amedai kwamba kila mmoja ana nafasi kubwa katika mchezo wa tennis duniani, na mafanikio ya mchezo huyo yameletwa na wachezaji wa jinsia zote.

Kauli hiyo ya Murray, imekuja kufuatia mpinznai wake Novak Djokovic, anaeshika nafasi ya kwanza duniani kwa wanaume, kuanika hadharani ushawishi wa kuhimiza wanaume kulipwa zawadi maradufu kuliko wanawake, kwa kisingizio cha kufanya kazi kubwa katika mchezo huo.

Djokovic alidai kwamba, wanaume wanapaswa kufanyiwa hivyo kutokana na kuwa na mvuto mkubwa zaidi katika ushindani, tofauti na wengine ambao wamekua wakijaribu kucheza baadhi ya michezo.

Kauli hiyo ilijaribu kuungwa mkono na aliyekua mkuu wa maandalizi ya michuano ya Indian Wells Masters, Rymond Moore kwa kutilia mkazo wa kuwataka wanawake kuwapigia magoti wanaume kutokana na juhudi zao za kuupaisha mchezo wa tennis duniani.

Hata hivyo kiongozi huyo hakuchukua muda mrefu, zaidi ya kujutia kauli hiyo kwa kutangaza kujiuzulu kutokana na wadau wa mchezo huo kumshinikiza afanye hivyo kwa kigezo cha kuwadhalilisha washiriki wa kike.

Wakati mambo yakiwa hivyo Murray mwenye umri wa miaka 28, amewataka mashabiki wake kutambua kwamba, mchezo wa tennis utaendelea kuwepo bila kujali jinsia, lakini akawakumbusha kuheshimu ama kupuuza maoni ambayo kila leo yamekua yakitolewa na wadau wa mchezo huo.

UEFA: Ufaransa Itakua Salama Wasalmin
Ozil: Wenger Ni Sababu Kubwa Kwangu Kujiunga Na Arsenal