Mwanamuziki kutoka Konde Music Worldwide Angella, amedokeza ujio wa wimbo wake mpya akiwa amemshirikisha boss wake, Harmonize kama sehemu ya kuendelea kusambaza upendo kwa mashabiki wake kwa muziki mzuri.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa Instagram Angella ameweka taarifa ya kuwa tayari uongozi wake umethibitisha kuwa nyota huyo atauachia rasmi wimbo huo mapema ifikapo Mei 13, 2022 yaani Ijumaa ya wiki hii, hivyo mashabiki na wadau wanaomuunga mkono wakae mkao wa kula.

“AM SO EXCITED!! #KIOO Ni Kati ya Project ambayo naamini licha ya kwenda Kuongeza Mchango mkubwa kwenye safari yangu ya muziki pia itaongeza mchango Kwenye Tasnia Nzima!!

Kama mlivyozoea Kunipokea Kila Wakati Naomba Mnipokee Tena Kwenye Hili!!, Confirmed!! “KIOO” Me Ft. TEMBO Harmonize,This Friday 13.5.2022″ ameandika Anjella.

Wabunifu watakiwa kutumia Ubunifu wao kuleta maendeleo
Kibwana Shomari hadi 2024 Young Africans