Klabu ya Chelsea imeripotiwa kuwa katika mazungumzo na uongozi wa SSC Napoli kwa ajili ya usajili wa mshambuliaji kutoka nchini Argentina, Gonzalo Higuain.

Baadhi ya vyombo vya habari vya mjini Naples yalipo makao makuu ya klabu ya SSC Napoli vimeripoti kwamba, meneja wa klabu ya Chelsea Antonio Conte ametoa msukumo kwa viongozi wake kufanya mazungumzo hayo kutokana na kuamini Higuain anatosha kuwa sehemu ya kikosi chake.

Taarifa hizo zimeelendelea kutanabaisha kwamba, Conte anamfikiria Higuain kufuatia kutokua na uhakika wa kumbakisha mshambuliaji kutoka nchini Hispania, Diego Costa, ambaye tayari ameshawasilisha ombi la kutaka auzwe kwenye klabu ya Atletico Madrid.

Wakati mazungumzo baina ya pande hizo mbili yakiendelea kama ilivyoripotiwa, thamani ya Higuain imeshatangazwa na rais wa klabu ya SSC Napoli, Aurelio de Laurentiis kuwa ni Euro milion 94.

Mpaka sasa Antonio Conte ameshakamilisha usajili wa mchezaji mmoja anayecheza nafasi ya ushambuliaji, Michy Batshuayi Tunga akitokea nchini Ufaransa alipokua akiitumikia klabu ya Olympique de Marseille.

Video: Makonda amezitaja adhari za uvutaji Shisha
Everton FC Yamuwinda Thomas Henry Alex "Hal" (Robson-Kanu)