Mshambuliaji Theo Walcott, kiungo Santi Cazorla pamoja na mabeki Hector Bellerin na Nacho Monreal hawakusafiri na kikosi cha Arsenal kilichoelekea nchini Bulgaria, tayari kwa mchezo wa wa kundi la kwanza wa ligi ya mabingwa barani Ulaya dhidi ya Ludogorets.

“Nacho, Hector, Santi na Theo hawakusafiri nasi,” meneja wa Arsenal Arsene Wenger aliwaambia waandishi wa habari katika mkutano maalum kuhusu mchezo wa leo.

“Ni wakati muafaka kwetu kuhakikisha tunashinda mchezo huu. “Tuna mchezo mgumu dhidi ya PSG tutakaocheza nyumbani siku zijazo, hivyo inatulazimu kupambana hapa ili tufikie lengo la kupata point tatu.

Arsenal na Paris St Germain, wanaongoza msimamo wa kundi A kwa kufikisha point saba kila mmoja, baada ya kushuka dimba mara tatu na tayari Arsene Wenger ameshawasisitiza wachezaji wake kuhakikisha wanashinda mchezo wa leo ili wajihakikishie nafasi ya kufuzu katika hatua ya 16 bora.

Ludogorets pamoja na FC Basel ambao watacheza na PSG hii leo, wana point moja kila mmoja.

Majuma mawili yaliyopita Arsenal walifanikiwa kuchomoza na ushindi wa mabao sita kwa sifuri dhidi ya Ludogorets, huku kiungo mshambuliaji kutoka nchini Ujerumani  Mesut Ozil akifunga mabao matatu (hat-trick).

Ivan Rakitic Atamani Kuwa Mtumishi Wa Guardiola
Video: Ziara ya Rais Magufuli Kenya