Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki nchini Uganda, Cyprian Kizito Lwanga amependekeza wafanyakazi ambao ni wakristo wakatwe asilimia 10 kwenye mishahara yao kila mwezi kama fungu la kumi na fedha hizo zisiwasilishwe kanisani.

Asakofu Lwanga amesema hayo kipindi cha misa ya jumapili iliyopita katika kanisa la Lubanga Cathedral na kusema kuwa wakristu wengi wakatoliki hawatoi zaka zao hali inayorudisha nyuma maendeleo ya kanisa.

”Tunamdanganya Mungu kwamba tunalipa zaka kwenye mishahara yetu, kipindi cha misa kama hivi, wakati wa kulipa zaka, wakatoliki huchukua chochote walichonacho mfukoni mwao na kutoa kama sadaka, lakini biblia inasema zaka ni asilimia 10 ya mshahara wako” Amesema askofu Lwanga.

Wakati akihubiri pia alitoa mfano wa Ujerumani ambako serikali huchukua jukumu la kukusanya zaka kila mwezi katika mishahara ya wafanyakazi na kuzipeleka kanisa husika.

”Ujerumani nilikokuwa hivi karibuni, kama mwajiriwa anatakiwa kupata milioni 1, Serikali humkata 100,000 na kubakiwa na 900,000 na utaribu huu unfanya kazi vizuri” amesema Askofu Lwanga.

Aidha bado haijajulikana kama waumini walikubaliana na wazo hilo la Askofu wao Cyprian Kizito Lwanga.

 

Alex Sandro awanyima usingizi Man Utd, Pogba ahusishwa
Rais Trump apigwa marufuku kutumia wimbo wa 'Happy'