Kikosi cha klabu ya soka ya Azam  FC Jumatano hii kinatarajia kusafiri kuelekea nchini Afrika Kusini kwa usafiri wa ndege wa shirikia la Fastjet kwa ajili ya kushiriki mchezo wao wa Kombe la Shirikisho dhidi ya klabu ya BIDVEST ukiwa ni mchezo wao wa kwanza wa kombe hilo.

Afisa habari wa Azam FC Jaffary Idd amesema kikosi hicho kimejiandaa vema tayari kwa mchezo wao huo na kitaondoka na jumla ya wachezaji 24 majira ya saa 5:00 kwa saa za Afrika Mashariki na wanatarajia kucheza mchezo wao huo Machi 12 mwaka huu.

Idd amesema kuelekea katika mchezo huo, mchezaji wao aliyekuwa majeruhi kwa kipindi kirefu Aggrey Moris amesharejea katika mazoezi ya kikosi cha kwanza kwa ajili ya kucheza mechi hiyo endapo kocha atampanga.

Licha Ya Kuambulia Kisago Cha 2-1, Twiga Stars Wajazwa Noti
Riyad Mahrez Atupiwa Chambo Wa Camp Nou