Bao lililofungwa na mshambuliaji chipukizi, Shaaban Iddi Chilunda limetosha kuipa Azam FC ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Zimamoto katika mchezo wa Kundi B Kombe la Mapinduzi.

Katika mchezo huo uliofanyika Uwanja wa Amaan mjini Unguja visiwani Zanzibar jioni ya leo, Chilunda alifunga bao hilo dakika ya 79 akimvisha kanzu kipa baada ya kupokea kwa ufundi kwa kifua pasi ya juu ya kiungo Salum Abubakar ‘Sure Boy’.

Mchezo wa pili wa kundi hilo unafuatia Saa 2:30 usiku huu kati ya mabingwa wa soka Tanzania bara Young Africans dhidi ya Jamhuri ya Pemba katika uwanja wa Amaan.

Bilic Amtuhumu Mwamuzi, Adai Man Utd Wamebebwa
Telegram yamkamatisha mtuhumiwa ugaidi Ujerumani