Msanii wa Rap Bongo, Chid Benz azidi kustaajabisha mashabiki wake mara baada ya kujitangaza kuja na kazi mpya alioifanya na marehemu 2Pac, sasa amesema anakuja na kazi nyingine akiwa amewashirikisha wasanii toka Marekani, Jay Z pamoja na Beyonce ambapo katika ngoma hiyo atamtoa Beyonce na kumuweka Linah Sanga.

Chid Benz amesema hayo alipohojiwa katika kipindi cha Friday Night Live cha EATV, na kuwataka mashabiki wakae tayari kwa ujio wa ngoma hiyo kali na wasani wa mbele.

Aidha  Chid Benz alitumia nafasi hiyo kumchana msanii Madee ambaye mara baada ya taarifa mitandaoni kuzagaa kuhusu Chid kufanya ngoma na marehemu 2Pac, Madee alitumia ukurasa wake wa Instagram kumponda kiana msanii  Chid Benz.

Katika kurasa wa Madee ameandika kuwa ”Ndio maana mimi sivuti hata sigara”. Sentensi ambayo Chib Benz imemkera kwani imeonesha uchochezi kuwa Chid Benz bado anajihusisha na madawa ya kulevya.

Kupitia mahojiano hayo Chid Benz aliwahahakishia mashabiki wake kuwa yeye ni mzima na kwa sasa hajihusishi na kutumia madawa ya aina yeyote kama ambavyo watu wengi wanadhani kutokana na kusambaa taarifa zake za kufanya kazi na wasanii hao tajwa.

 

 

Trump apanga kuwaelewesha Korea Kaskazini kwa kitu kimoja tu
Msuva amtaja Samatta kuwa chachu ya mafanikio yake kisoka