Ikiwa ni siku chache tu zimepita tangu klabu ya Yanga iadhibiwe faini ya shilingi laki mbili 200,000/=, kwa kuingia uwanjani kwa kupitia mlango ambao sio rasmi, kitendo hicho kimejirudia tena hapo jana wakati wa mechi dhidi ya Simba.

Yanga waliingia kwenye uwanja wa taifa kwa kutumia mlango usio rasmi huku pia wakitumia basi dogo aina ya Coaster wakiacha basi lao likiingia bila wachezaji. Jambo ambalo walilifanya pia kwenye mechi dhidi ya Coastal Union kwenye uwanja wa Mkwakwani Tanga na kuadhibiwa na TFF.

Aidha, Yanga ndio walikuwa wa kwanza kufika uwanjani hapo, huku gari kubwa lililokuwa limebeba baadhi ya wachezaji wake likipitiliza sehemu lililopozoeleka kupaki na kwenda kusimama karibu na mlango wa kuingilia mashabiki wa Simba.

Kitendo hicho kilitokea hapo jana ambapo gari aina ya Toyota Coaster liliingia uwanjani huku likiwa limebeba wachezaji wa kikosi cha kwanza huku wale wa akiba wakiwa kwenye basi kubwa.

Kitendo hicho cha wachezaji wa Yanga kuingilia mlango usio rasmi kilizua kelele kwa mashabiki wa Simba, huku meneja wa Yanga Nadir Haroub na kocha wa makipa Juma Pondamali wakiwafuata na kuingilia mlango huo.

Hukumu kesi ya Malkia wa Tembo imeiva
Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Februari 17, 2019