Waziri wa Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar(SMZ) Balozi Ali Abeid Aman Karume amewataka Watanzania kutembelea sehemu za vivutio vya utalii na kuondokana na dhana kwamba utalii unafanywa na wageni tu.

Ameyasema hayo Wilayani Mbozi Mkoa wa Songwe wakati alipotembelea eneo la urithi na uhifadhi ambapo kulidondoka Kimondo chenye uzito wa tani 12.

“Nimefurahishwa sana na historia ya Kimondo hiki ni vyema Watanzania wengi zaidi wakatenga muda kuja kujifunza hapa, ni jambo la kujivunia kidunia kuwa sehemu ya nchi zanye Vimondo vizito zaidi duniani”Amesema Balozi Karume.

Balozi Karume aliongozana na Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brig. Jenerali Mwangela, Naibu Waziri, Anthony Mavunde na Naibu waziri wa Vijana SMZ, Lulu Mshamu kukagua maandalizi ya mwisho ya uzinduzi wa Mbio za Mwenge Kitaifa zinazotarajiwa kuzinduliwa tarehe  2, 4, 2019 Mkoani Songwe.

Video: NEC yapuliza kipenga uchaguzi wa Arumeru, Makonda achafua hewa
Dudu Baya aipigia magoti familia ya Marehemu Ruge, Serikali ‘mnisamehe’