Afisa Mtendaji Mkuu wa Klabu Bingwa Tanzania Bara Simba SC Barbara Gonzalez amekiri kupokea malalamiki ya Mkuu wa Idara ya Habari ya klabu hiyo Haji Manara.

Barbara ametoa mrejesho huo, kufuatia kutuhumiwa kuwa na chuki binafsi dhidi ya Manara, ambaye amesambaza sauti yake kwenye mitandao ya kijamii, akieleza namna anavyochukiwa na bosi wake.

Kiongozi huyo amesema kwa sasa sio muda muafaka kwake kujibu tuhuma hizo, na badala yake ameamua kujikita kwenye maandalizi ya mchezo wa Fainali Kombe la Shirikisho *ASFC* dhidi ya Young Africans.

“Nimesikia madai ya Msemaji wetu Haji Manara, kwa sasa lengo letu kubwa ni ushindi mechi ya fainali Kombe la Azam Shirikisho na mengine yatafuata,” amesema Barbara.

Simba SC itatetea taji la ASFC kwa kuikabili Young Africans, Jumapili (Julai 25), Uwanja wa Lake Tanganyika mkoani Kigoma.

Kilo 164 ya samaki wamekufa ufukwe wa Dar es Salaam
Bumbuli: Ndugu wakigombana shika jembe ukalime