Mtu mmoja amefariki na wengine sita kujeruhiwa baada ya Basi la kampuni ya Newforce kuangua kwenye korongo eneo la msimba barabara kuu ya Iringa – Morogoro.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Fortunatus Musilimu amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema mwili wa marehemu umehifadhiwa hospital ya ST. Kizito katika Mji wa Mikumi mkoani Morogoro, huku majeruhi wakiendelea kupatiwa matibabu katika hospitali hiyo.

Amesema chanzo Cha ajali ni uzembe wadereva la basi hilo la New Force aliyekuwa akijaribu kuyapita magari mengine yaliyopo mbele yake bila kuchukua thadhari.

'Johnson's Baby Powder' yashukiwa kusababisha kansa
Polisi yajipanga kukabiliana na Dawa za kulevya