Msanii wa nyimba za Bongo fleva, Ben Pol ambaye hivi karibuni kuna tetesi kuwa yupo kimahusiano ya kimapenzi na msanii wa maigizo ya kuchekesha Ebitoke kutoka Timamu media, Ben Pol amekuwa akidhibitisha kuwa ni kweli kile ambacho wanakiona mashabiki wa Ebitoke na Benpol na sio maigizo.

Kutokana na mtindo uliotanda siku hizi miongoni wa wasanii wa Bongo Muvi na Bongo Fleva kutafuta umaarufu kwa kupitia kiki, basi ilifikiriwa kuwa wasanii hawa wawili kuwa katika mahusiano ni moja ya maisha waliochagua kujitafutia umaarufu zaidi kwa kiki hiyo.

Taarifa zilizozagaa mtaondoni hivi karibuni zinadai kuwa msanii Ben Pol, amelipwa shilingi milioni 3 na Timamu media ili kujiweka karibu na msanii Ebitoke.

Hivyo Ben Pol amekanusha tetesi za kusema amelipwa na Timamu media ili kujiweka karibu na msanii wa maigizo ya vichekesho Ebitoke, na ameeleza kuwa kila kitu ambacho kimetokea kwenye maisha yake akiwa na Ebitoke hakuna Kilichotengezwa huku akidai yote yalikuwa ni maisha yake halisi.

TFF yaipangua ratiba ya Ligi daraja la kwanza 2017/18
Mabalozi nchi za Ulaya na Marekani walaani mauaji nchini Kenya