Mwanamuziki mahiri na muwakilishi wa kundi maarufu la muziki kutoka nchini Kenya ‘Sauti Sol’ Bien-Aime Baraza ametangaza kubadilisha mfumo wa matumizi yake ya mitandao ya kijamii, kutokana na kile alichodai kuwa mitandao hiyo ni sawa na sehemu ya sumu.

Bien ameutumia ukurasa wake wa mtandao wa twitter kubainisha dhamira yake ya kuacha mitandao baada ya kutafakari maisha yake kwa muda mrefu.

“Baada ya kujitazama kwa muda mrefu kwenye kioo, nimeamua kubadili njia zangu. Mtandao ni mahali pa sumu sana na ninataka tu kuchukua hatua, Kuna tabia nyingi ambazo nilizichukua na mwaka huu naziacha, Nataka tu kupumzika na kurudi nyuma,” alisema.

Akiongeza kuhusu uamuzi huo, Bien alisema kuwa anajua mchakato wa mabadiliko hautakuwa rahisi, lakini amejipanga kwa safari ndefu inayokuja na kukiri kufikia hatua ya kuacha hata matumizi ya vileo.

Kufuatia uamuzi wa nyota huyo, aliungwa mkono na watu mbali mbali licha ya kuwepo kwa waliompinga kiasi cha kubashiri kuwa hatoweza kutekeleza mpango huo.

Kanye West atangaza lingine kubwa mwaka huu
Filamu ya Bongo yawaogopesha Wakenya