Ushindi wa rais mteule wa Marekani Donald Trump, unampa shaka meneja wa klabu ya Swansea City Bob Bradley, kuhusu uwezekano wa taifa hilo kushinda nafasi ya kuwa mwenyeji wa fainali za kombe la dunia za mwaka 2026.

Shirikisho la soka nchini Marekani tayari limeshaonyesha nia ya kuwasilisha maombi ya kuwa mshiriki katika kinyang’anyiro cha kuwania nafasi ya kuandaa fainali hizo.

Mbali na upande wa soka pia hofu nyingine imetanda kwa jiji la Los Angeles kupata nafasi ya kuwa mwenyeji wa michezo ya Olimpiki ya mwaka 2024, kutokana na ushindi wa Trump.

Marekani inahofiwa kukosa nafasi ya kuchaguliwa kuwa mwenyeji wa michuano hiyo kutokana na sera za Trump ambazo zimepokelea kama ukandamizaji wa haki za binaadamu dhidi ya mataifa mengine.

Bradly ameonyesha wasiwasi kwa nchi yake ya Marekani kukosa nafasi ya kuwa mwenyeji wa fainali za kombe la dunia, kufuatia kauli ya raisi huyo mteule ya kujenga ukuta katika mpaka wa nchi hiyo dhidi ya Mexico.

Akitolea mfano wa jambo hilo kwa kuigusa nchi ya Urusi ambayo inaendelea na maandalizi ya fainali za kombe la dunia za mwaka 2018, Bradly ambaye alikiongoza kikosi cha Marekani hadi kwenye hatua ya 16 bora ya fainali za mwaka 2010, amesema imekua ni vigumu kwa taifa hiyo kuzungumzwa kwa mazuri duniani kutokana na uhusiano mbaya uliopo dhidi ya nchi jirani ya Ukraine.

Image result for Bob Bradley - sky sportsBob Bradley

Amesema imekua ni bahati kwa Urusi inazungumzwa kwa mabaya kuhusu ushirikiano wake na Ukraine ikiwa tayari imeshapata nafasi ya kuwa mwenyeji wa fainali za kombe la dunia, lakini anaamini kwa Marekani itakua ni vigumu endapo Mexico watatenganishwa na ukuta ambao huenda ukajengwa wakati wa utawala wa Trump.

Jambo lingine ambalo linampa wasiwasi Bradly wa kuiona Marekani inakosa nafasi ya kuwa mwenyeji wa fainali za kombe la dunia, ni sera ya kutaka kuwafukuzwa watu weusi wanaoishi nchini Marekani kwa kigezo cha kupora kazi za wenyeji, jambo ambalo anaamini litatazamwa kama ukiukwaji wa haki za kibinaadamu.

Hillary Clinton aponea chupuchupu kwenye mikono ya Donald Trump
Mfumo Wa Vincenzo Montella Kumkimbiza Bacca