Nahodha na Mshambulaiji wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC John Raphael Bocco amesema suala la kufunga ama kutokufunga katika michezo anayopata nafasi ya kucheza linapangwa na Mwenyezi Mungu.

Bocco ametoa kauli hiyo kufuatia lawama anazoangushiwa na baadhi ya Mashabiki na Wanachama wa Simba SC, kufuatia timu yao kupoteza mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Mbeya City, huku akikosa nafasi kadhaa.

Mshambuliaji huyo aliyemaliza Ligi Kuu msimu uliopita akiwa kinara wa mabao, amesema anaamini muda ukifika atafunga na kilichotokea jana ni mipango ya Mungu.

“Suala la kufunga ni bahati, muda ukifika na Mungu akipanga nifanye hivyo nitafunga, kikubwa ni kuwa miongoni mwa mastaa wanaocheza Simba SC, nikipata nafasi nitapambana kwa ajili ya kuitetea timu itete mataji.” amesema Bocco

Bocco amekua hapati nafasi ya kuanza kwenye kikosi cha kwanza cha Simba SC, kufuatia Mshambuliaji Meddie Kagere kupewa nafasi mara kwa mara na kocha Franco Pablo Martin.

Ziara ya Rais Mwinyi UAE imezaa matunda
Rais Samia afanya uteuzi