Bondia Shaban Kaoneka amevitupia lawama Vyombo vya habari Tanzania kwa kushindwa kumpa nafasi kama mshindi wa pambano lake na Karim Mandonga, na badala yake mpinzani ameonekana kuwa bora zaidi yake.

Wawili hao walipambana Julai 30 mjini Songea mkoani Ruvuma katika Pambano la utangulizi, kabla ya Bondia wa Tanzania Seleman Kidunda na Erick Tshimanga Katompa kupapatuana ulingoni.

Kaoneka aliyemshinda Mandonga katika Raund ya nne, amezungumza na Dar24 Media na kudai kuwa, vyombo vya habari vimemtupa na havitaji kumpa nafasi, huku akishngaa namna vinavyompa fursa Bondia Karim Mandonga.

“Mandonga amepata bahati kuliko mimi, waandishi wa habari wakati mwingine naona kama mnakuwa wanafiki, hamjaniita hata ofisini kwenu kunihoji, mbona Mandonga mnamfanyia surprise nyingi, mimi niliyeshinda nakuwa masikini, aliyepigwa anakuwa tajiri,” amesema Shabani Kaoneka.

Karim Madonga kwa sasa amekua maarufu kutoana na kupewa nafasi kubwa katika baadhi ya vyombo vya habari, huku ikisemekana ameanza kuingia Dili na baadhi ya Makampuni na kujiingizia kipato.

F.B.I wafanya upekuzi makazi ya Rais
Wengi waikimbia polio wiki ya unyonyeshaji