Rapa anayeunda kundi la Weusi, Bonta ambaye anafahamika kwa mashairi yenye uanaharakati na ufuatiliaji wa historia ameeleza kile anachokifahamu kama sababu iliyopelekea Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kukataa kuonana na Muhammad Ali alipotembelea Tanzania mwaka 1980.

Bonta

Bonta

Bonta amesema kuwa Bondia huyo alikuja na ujumbe maalum kutoka nchini Marekani akitaka kuishawishi Tanzania kutoshirikia mashindano ya Olympic nchini Urusi lakini Mwalimu Nyerere ambaye alikuwa Rais wakati huo, alimtuma Waziri Mkuu wa wakati huo, Salim Ahmed Salim kukutana na Bondia huyo.

Alisema Mwalimu Nyerere hakutaka kuwa katika upande wowote kati ya nchi hizo kwani wakati huo kulikuwa na vita baridi kati ya nchi hizo.

“Enzi hizo waziri mkuu alikuwa Salim Ahmed Salim na lengo la kufika hapa mashindano ya Olimpiki yalikuwa yanafanyika Urusi na yeye akiwa kama Mmarekani alitumwa na ujumbe kutoka Marekani akawa ameuleta Tanzania na kwa bahati mbaya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alikataa kuonana naye,” Bonta aliiambia Jembe Fm.

“Ni kwasababu taifa letu la Tanzania lilikuwa ni non alignment (hatujihusishi na pande yoyote ile) Marekani au Russia enzi hizo ikiwa USSR kwasababu kama unakumbuka walikuwa na vita baridi. Sasa Muhammad Ali alikuwa ametuletea ujumbe watanzania kwamba tusiende kushiriki kwenye Olimpiki inayofanyika Russia tugomee mashindano yale,” aliongeza Bonta.

Historia inaeleza kuwa kabla ya kuondoa nchini, Muhammed Ali akifika katika hotel ambayo hivi sasa ni Hayyat Regency, iliyoko jijini Dar es Salaam na umati mkubwa ulifurika kumuona.

Muhammad  Ali atazikwa kesho nyumbani kwao Louisville, Kentucky nchini Marekani.

Je, kwenye hili Bonta kapatia historia?

Mohammed Kiganja: Mamluki Marufuku Umitashumta
Video: Simu yako itazimwa na TCRA? Tigo wanakuarika ukajipatie simu ya Buree...