Mtoto Bradley Lowery aliyekuwa na tatizo la kiafya lililogusa nyoyo za wengi duniani amefariki dunia akiwa na umri wa miaka sita .

Bardlaye ambaye ni shabiki wa klabu ya Sunderland alikuwa anaugua ugonjwa ambao unafahamika kama ‘Neuroblastoma’ (aina nadra ya saratani) tangu alipokuwa na umri wa miezi 18.

Aidha, aliongoza wachezaji wa England kuingia uwanjani Wembley wakati wa mechi ya kufuzu kwa Kombe la Dunia dhidi ya Lithuania.

Bradley alifanywa kuwa kama nembo wa klabu hiyo hata kuwa rafiki wa karibu na mshambuliaji wa klabu hiyo Jermain Defoe.

Wazazi wa Bradley wamethibitishwa kifo chake kupitia mitandao ya kijamii.

“Alikuwa shujaa wetu na alipigana sana lakini alihitajika kwingine. Hatuna maneno ya kueleza jinsi tulivyohuzunishwa na kifo chake.”

Bradley alipendwa na maelfu ya watu na alipokea kadi 250,000 za kumtakia heri wakati wa Krismasi, kutoka kwa watu mataifa ya mbali kama vile Australia na New Zealand.

Wakati wa uhai wake, wahisani mbali mbali walichangisha zaidi ya £700,000 kulipia matibabu yake New York mwaka 2016, lakini madaktari waligundua kwamba saratani yake ilikuwa imeenea sana na hangeweza kutibiwa.

 

Mnamo Disemba, Wazazi wake Bradley, Gemma na Carl, kutoka Blackhall Colliery, Durham, walisema mtoto wao amebakia na miezi kadha tu ya kuishi.

Miezi minne baadaye, walifahamishwa kwamba jaribio la mwisho kabisa la kumtibu lilikuwa limefeli.

Serikali yapunguza gharama za dawa, vifaa tiba na huduma za afya
Leceister City Wasajili Mtu Wa Kazi Kutoka Spain