‘Video Queen’ maarufu nchini Tanzania, Agness Gerald maarufu kama Masogange amefariki dunia katika hospitali ya Mama Ngoma iliyopo Mwenge, jijini Dar es salaam, jioni ya leo Aprili 20, 2018

Akithibitisha taarifa hizo ndugu wa karibu na marehemu, Dick Sound amesema mwili wa marehemu unasafirishwa jioni hii kwenda kuhifadhiwa mochwari katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Akielezea sababu za kifo hicho, shangazi yake Masogange amesema amesumbuliwa na pumu kwa muda mfupi hali iliyopelekea kulazwa katika hospitali ya Mama Ngoma hadi mauti ilipomkuta.

Amesema awali hakuwahi kupata ugonjwa huo na hadi asubuhi ya leo hali yake haikua mbaya na kifo chake kimewashtua na kuwaachia majonzi makali.

Awali, Masogange alishindwa kuhudhuria Mahakamani kwa wiki tatu zilizopita kusikiliza kesi iliyokuwa ikimkabili kabla ya kesi hiyo kutolewa hukumu wiki iliyopita.

Watu mbali mbali wakiwemo wanasiasa na Mastaa mbalimbali wa muziki na waigizaji wa filamu wameeleza kushtushwa na  kifo cha Masogange na wametoa pole kufuatia taarifa hizo.

Dar24 Media inatoa pole kwa familia yake katika kipindi hiki kigumu.

Video: Mrema amjibu Polepole, amtaka arudi darasani
Jalada kesi ya Akwilina lafungwa, DPP atoa onyo kali