Moto mkubwa umeteketeza jengo moja la ghorofa la ‘Grenfell Tower’ lililopo  katika barabara ya Latimer, London, ambapo hadi sasa taarifa zinaeleza kuwa baadhi ya watu bado wamekwama ndani ya jengo hilo.

watu walio shuhudia tukio hilo wanasema, moto huo umeleta mshituko mkubwa hali iliyosababisha baadhi ya watu kushindwa kutoka katika makazi yao.

Jeshi la Polisi jijini London limesema kuwa hadi sasa imebainika kuwa watu wawili ambao wameathirika na moshi wa moto huo na wanapata matibabu huku idadi ya kamili ya watu waliokwama ndani ya jengo hilo bado haijulikani.

Moto huo unaendelea kuunguza jengo hilo hadi sasa huku vikosi vya uokoaji na zima moto takriban 200 vikiendelea na kazi hiyo huku malori 40 ya kuzima moto yakielekezwa eneo hilo na idara ya zimamoto jijini Londoni ili kuongeza nguvu.

?Live: Yanayojiri Bungeni Dodoma leo Juni 14, 2017
Video: Wataka Mkapa, JK washitakiwe, Lowassa akoleza moto wa mchanga