Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi, Abdallah Bulembo, ameongoza vikao vya ndani vya chama cha mapinduzi CCM kwaajili ya kusimamia vizuri uchaguzi unaoendelea ndani ya chama hicho.

Bulembo amesema kuwa ili chama hicho kiendelee kuiongoza Tanzania lazima kisimamie misingi ya demokrasia katika chaguzi zake za ndani ili kiweze kutoa viongozi thabiti , imara na wenye uzalendo wa kweli.

Aidha, katika ziara yake ya kutembelea matawi mbali mbali mikoani, Bulembo amesema CCM ni chama kikubwa na chenye heshima kubwa barani Afrika na dunia kwa ujumla hivyo amewataka viongozi wote waliopo ndani ya chama hicho kutimiza majukumu yao.

“Katika uchaguzi unaoendelea ndani ya chama chetu ngazi ya mashina kuna haja kubwa ya kuutizama kwa jicho la tatu ili tuweze kupata viongozi wazalendo ambao wataendelea kukijenga chama chetu,”amesema Bulembo.

 

Picha: Kuapishwa kwa IGP mpya Ikulu Dar es salaam
WCB wapigwa marufuku kuingia klabu usiku

Comments

comments