Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Young Africans Hassan Bumbuli, amesema kurejea kwa mabeki Abdallah Shaibu ‘Ninja’ na Yassin Mustafa, kutatoa nafasi kwa benchi la ufundi la klabu hiyo kuwa na wigo mpana wa kufanya maamuzi ya nani aanze kwenye kikosi cha kwanza dhidi ya Simba SC.

‘Ninja’ na Yassin Mustafa wamerejea kwenye mazoezi ya pamoja na wachezaji wengine wa Young Africans yanayoendelea kwenye viwanja vya Avic Town, Kigamboni jijini Dar es salaam.

Bumbuli amesema: “Maendeleo yetu ni mazuri, na wachezaji wetu Abdallah Shaibu Ninja na Yassin Mustapha waliokuwa majeruhi kwa takribani wiki 8 wamerejea, hivyo kutakuwa na chaguo pana kwa benchi la Ufundi katika nafasi ya Ulinzi”.

Kuhusu mchezo wa Jumamosi (Julai 03), Bumbuli ametanabaisha kuwa utakuwa mchezo wa kawaida kama ilivyo michezo mingine.

Amesema kwao kama Young Africans hawatokuwa na Presha kwenye mchezo huo, hivyo watapambana kama ilivyo kawaida yao, tofauti na Simba SC ambao watahaha kusaka alama tatu ili kutimiza ndoto zao za ubingwa msimu huu.

“Ni mchezo wa kawaida Kama ilivyokuwa mchezo mingine kwani wachezaji wanacheza 11 kila upande, isipokuwa hu ni mcheczo wa watani wa jadi, na wenzetu watakuwa na presha kubwa kuliko sisi kwa sababu wanataka kutanganza Ubingwa katika dhidi yetu”

“Kuhusu Kauli ya Haji Manara kuwaomba TFF ikiwezekana walete Kombe Uwanjani Yale ni maneno na sisi tukiamua kuongea tuna maneno makali yeye asubili mpira ni dakika 90, na bila makandokando hawawezi kutufunga na zile goli 4 anazosema walitufunga ni kwa sababu ya kimazingira tayari kulikuwa na baadhi ya wachezaji wetu kuwa upande wao,” amesema Bumbuli.

Simba SC endapo itashinda ama kutoa sare dhidi ya Young Africans itajitengenezea mazingira ya kutwaa ubingwa wa nne mfululizo.

Kwa sasa Simba SC inaongoza msimamo wa Ligi Kuu kwa kuwa na alama 73, akifuatiwa na Young Africans yenye alama 67 na Azam FC inashika nafasi ya tatu kwa kumiliki alama 64.

Viongozi Simba wavamia mazoezi Bunju
Kutana na kijana aliyerudia darasa la kwanza kwa miaka 15, ana ndoto ya kuwa Rais