Rais wa zamani wa Zimbabwe, Robert Mugabe ametakiwa kufika katika kamati ya bunge mwezi ujao kujibu madai ya upotevu wa mapato ya mgodi wa madini ya almasi mwaka 2016.

Kamati hiyo ya bunge imemtaka kufika na kujieleza Mei 9 mwaka huu, witio ambao bado unatia shaka kama utaitikiwa na Mugabe.

Mwenyekiti wa kamati hiyo, Temba Mliswa amesema kupitia kituo cha habari cha taifa hilo kuwa kamati imefikia uamuzi huo baada ya kufanya tathmini ya madini hayo katika eneo la Marange.

Mwaka 2016, mapato ya $15 bilioni ya almasi yaliibiwa. Lakini Serikali haikumpata aliyesababisha upotevu huo.

Inadaiwa kuwa makampuni mengi ikiwemo ya kutoka China pamoja na jeshi la nchi hiyo, walipewa mikataba mikubwa ya kuchimba madini katika migodi ya almasi.

Jicho la kamati hiyo ya Bunge kwenye sekta hiyo kunatokana na madai kuwa suala la madini ya almasi katika nchi hiyo limekuwa kitendawili cha ubadhilifu wa mali za umma.

Jalada kesi ya Akwilina lafungwa, DPP atoa onyo kali
Video: Serikali yathibitisha hakuna upotevu wa Trilioni 1.5