Bunge la Brazil limepiga kura kupinga mashtaka ya rushwa yanayomkabili Rais wa nchi hiyo, Michel Temer hivyo hatua hiyo imemuepusha kufikishwa mbele ya mahakama kuu, hatua ambayo ingesababisha aondolewe madarakani.

Wabunge wa Brazil wameungana na kuyatupilia mbali mashtaka ya rushwa yaliyokuwa yanamkabili rais huyo hivyo kumuepusha kuwa rais wa pili wa Brazil kuondolewa madarakani katika kipindi cha mwaka mmoja.

Temer amesema kuwa uamuzi uliopitishwa na wabunge sio ushindi  wa mtu binafsi lakini ni ushindi wa demokrasia katika nchi inayofuata utawala wa sheria na Katiba na inayoheshimu haki za binadamu.

Aidha, Wapinzani nchini humo walitaka kulipiza kisasi kutokana na rais Temer kuingia madarakani mwaka mmoja uliopita baada ya wafuasi wake bungeni kupiga kura ya kutokuwa na imani na rais aliyemtangulia hapo awali Dilma Rousseff kwa kuvunja taratibu za bajeti.

Hata hivyo kunusurika kwa rais huyo kwa sasa siyo mwisho wa matatizo yake kwani bado inawezekana kwa mwendesha mashtaka mkuu nchini Brazil kumfungulia mashtaka mengine ya rushwa.

Maalim Seif akabidhisha barua kwa spika kufukuza wabunge wawili CUF
Manji na wenzake wazidi kusota jela