Mgombea wa urais kupitia chama cha mapinduzi (CCM), Dkt. John Magufuli amewaomba wakazi wa Nzera, wilaya ya Geita mkoani Geita kumpa kura kwa miaka mitano mingine ili kumalizia vijiji vyote kuweka umeme ikiwemo vijiji vya mkoani hapo.

Akizungumza na wakazi hao katika mkutano wa kampeni za kuwania urais, dkt. Magufuli amesema serikali yake imefanya kazi kubwa katika suala la umeme na endapo watapewa kura watahakikisha kuwa ndani ya miaka miwili umeme utakuwa umesambaa maeneo yote.

“Nimezungumza hili kwa ujasiri mkubwa, umeme sasa upo tunajenga bwawa kubwa la umeme la Nyerere litakuwa linatoa umeme megawati 2115, huu umeme utaunganishwa” amesema Magufuli.

Dkt. Magufuli anatarajiwa kuendelea na kampeni zake mkoani Geita, kesho Septemba 9.

Corona yavamia kambi Manchester City
Mwamba amerudi, kupambania taji 2020/21