Rapa anayewakilisha Ilala, Chid Benz aka King Kong au Chuma amedai kuwa muziki wa kizazi kipya unaofanywa hivi sasa umekuwa kazi ya hatari, tofauti na ilivyokuwa hapo awali.

Chid Benz ambaye alianza kuteka mawingu ya mkondo mkuu wa muziki miaka takribani 20 iliyopita, amesema ingawa enzi hizo watu walikuwa wakiamini kuwa muziki una mambo mengi ya kiswahili/kishirikina, wakati huu hali imekuwa ya hatari zaidi.

“Wanasema sasa hivi muziki umetanuka, zamani ndio ulikuwa uko kiswahili sana. Lakini nahisi kama sisi zamani ndio tumeuenjoy, ila sasa hivi ndio muziki umekuwa kazi ya hatari. Falsafa yangu inasema, ‘it’s either you Wasafi ama Wachafu’. Kama hauko katika hizo mbili, that means (ina maana) unaondoka… unaondolewa,” aliiambia Pro24 DJ hivi karibuni.

“Wanakuondoa, unabakia  katikati na wanapata nafasi ya kusema huyu ndio wa kumchangia. Kwa hiyo kuweni makini… waandishi, watangazaji wanakufa kiajabu ajabu,” aliongeza.

Katika mahojiano hayo, rapa huyo alitaja baadhi ya wasanii ambao alidai kuwa wanategemea nguvu za kishirikina lakini wengi wao hivi sasa wamepotea kwani nguvu hizo huwa za msimu.

Mshindi huyo wa Tuzo za Kili aliyewahi kunyakua tuzo tatu kwa mpigo kupitia muziki wake, hivi sasa anaonekana kurejea katika hali yake ya kawaida baada ya kupambana na ulaibu wa matumizi ya dawa za kulevya kwa kipindi kirefu.

Majaliwa awatangazia kiama wanaoteka watoto
Mahakama yafuta wadhamini timu Lipumba, Maalim... CUF kama zamani

Comments

comments