Msanii wa Hip Pop Bongo, Chid Benz amjia juu msanii mwenzake wa Bongo Fleva, Chin Bees na kumtaka msanii huyo kubadilisha jina la muziki analolitumia.

Chid Benz ameona kuna mfanano mkubwa kati ya jina lake na jina la msanii Chin Bees hivyo amemtaka alibadilishe kwani hata aina ya mziki wanayoifanya wawili hao ni tofauti, amesema Chid Benz.

Chid Benz amezungumza amesema “Siku moja nimeona Shetta anamuangalia instagram nikamuuliza huyo ni nini?, akaniambia ni Chin Bees, nikamuuliza anafanya muziki gani, akaniambia Bongo Fleva!. Sisemi kwa ubaya ila sikuelewa ile style anayofanya yeye ni tofauti sana na mimi mtu mzima mwenye hit kama 32 najua nikiingia kwenye stage nachapa tu,”

“Huyo Chin Bees ana single hata saba kweli?, atafute jina lingine,” amemaliza kwa kusema.

Chid Benz amezungumza hayo alipohojiwa katika kipindi cha  Planet Bongo katika  East Africa Radio.

 

John Raphael Bocco Aongezwa Stars
Alikiba atangazwa kuwa Mkurugenzi wa kampuni ya Rockstar4000