Msanii mkongwe wa Hip Hop nchini Rashid Makwiro maarufu kama Chid Benz anashikiliwa na jeshi la polisi mkoani Dodoma kwa tuhuma za kukutwa na dawa za kulevya aina ya Heroine na hii ni mara ya tatu kwa msanii huyu kukumbwa na sakata hili.

Kamanda wa Polisi Mkoani Dodoma, SACP, Giless Muroto amethibitisha kukamatwa kwa Chid Benz mkoani kwake.

“Ni kweli Chidi Benz mnamo tar 30/12/2017, tulimkamata akiwa yeye na mke wake na vijana wawili. Tumemkamata akiwa na dawa za kulevya zidhaniwayo kuwa ni Heroine. jalada lake lipo tayari kwa Mwanasheria wa wa serikali linafanyiwa uchunguzi na muda wowote watapelekwa mahakamani”.

Hata hivyo Muroto amesema taarifa kamili zitatolewa hapo kesho, ila mpaka sasa watuhumiwa hao wapo mahabusu.

Mjumbe wa Kamati Kuu Chadema atimkia CCM
Waliojichubua na wenye michirizi mwilini kukosa ajira

Comments

comments