Beki na Nahodha wa Mbeya Kwanza FC Salum Chuku, amefunguka baada ya timu hiyo kulazimisha sare ya mabao 2-2 dhidi ya Polisi Tanzania, katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara mzunguuko wa tano.

Mchezo huo ulichezwa jana Jumatatu (Novemba Mosi) Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya, ambapo wenyeji Mbeya Kwanza FC walitanguliwa kufungwa mabao 2-0, kabla ya kusawazisha kipindi cha pili.

Chuku amesema kikosi chao kina wapambanaji wa kutosha, na siku zote wanapoingia Uwanjani wanatambua Mashabiki wao wanahitaji kitu gani, ndio maana hawakubali kufungika kirahisi.

“Tunajua Nini mashabiki Wetu na wana Mbeya wanakihitaji nasi tunaumia kwa tunachokipata tuzidi kuombeana heri mchezo ujao tutapata hitaji Letu” amesema Salum Chuku.

Mbeya Kwanza FC inayoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara kwa mara ya kwanza msimu huu 2021/22, ipo nafasi ya sita ikiwa na alama 07.

Klabu hiyo ya jijini Mbeya ni miongoni mwa klabu za Ligi Kuu ambazo bado hazijakubali kupoteza mchezo wa Ligi hiyo hadi sasa.

Antonio Conte meneja mpya Spurs
Antonio Conte aahidiwa mabilioni ya shilingi