Zaidi ya chupa za damu 550 zinahitajika mkoani Njombe ili kukidhi mahitaji yote kwa mwezi ambapo jumla ya chupa 470 tu kati 601 ndio zinazokusanywa huku kukiwa na upungufu wa chupa 131 hali inayowalazimu waratibu wa damu salama kuiomba jamii kujitokeza katika zoezi la uchangiaji ili kuwasaidia wenye mahitaji hayo.

Hayo yamesemwa na Mratibu wa Damu Salama Mkoa wa Njombe, Prisca Ndiasi wakati wa zoezi la uchangiaji wa damu, ambapo amesema kuwa wanalazimika kuendesha zoezi hilo muhimu Kutokana na Upungufu Mkubwa wa Damu.

“Mpaka sasa tunauwezo wa kukusanya chupa 470 hadi 480 kwa mwezi kwa hiyo bado tunauhitaji tunaiasa jamii na wananchi wa Njombe kujitokeza na kuchangia damu kwa hiari kwa kuwa bado tuna uhitaji mkubwa,” amesema Ndiasi

Kwa kuona umuhimu huo Ili kukabiliana na tatizo la upungufu wa damu Kwa wagonjwa mkoani Njombe Jeshi la Polisi mkoani humo limeungana na Wakristu wa Dhehebu la Waadventista wasabato Kuchangia Damu Baada ya Wakristo Hao Kutekeleza Zoezi Hilo Disemba 26 Mwaka Huu.

Kwa upande wake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe, Renatha Mzinga Katika Bwalo la Jeshi hilo wamechangia damu Ili Kuunga Mkono Jitihada Hizo Kwa ajili ya Kusaidia Wagonjwa wenye mahitaji ya Damu.

 

Live: Rais Magufuli akutana na viongozi wa TUCTA, NSSF, PSSSF na SSRA kuhusu KIKOKOTOO
Video: Lissu achafua hali ya hewa Chadema, Simbachawene ampa kichapo dereva wa lori

Comments

comments